President of United Republic of Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete has said Zambia and Africa have lost a brave woman who helped a lot Zambia and the whole continent during independence struggle.

Tanzania’s President, Dr Jakaya Mrisho Kikwete

The Late Betty Kaunda

President Kikwete said that in the statement released by Directorate of Presidential Communications yesterday, as the President was sending condolences to the Former President of Zambia, Keneth Kaunda following death of his beloved wife, Betty Kaunda.

Dr Kikwete said the African continent and Zambia will always remember her as a woman who participated fully in fostering Zambian development and African development at large.

“I have been saddened and shocked by the information of Betty’s death happened this week in Harare, Zimbabwe, where she was visiting her daughter, Mama Musata Kaunda Banda. Her death is not only a shock to you, your family or Zambian citizens but also to all Africans.”

President Kikwete said he is together with all family members and Zambians in the difficult time they face following death of Betty Kaunda.

Betty Kaunda was born in 1928, got married to Keneth Kaunda in 1946 died on Tuesday with the age of 84 years old.

——————————————————————————————————————————————————————————————————————————————————————
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Mstaafu wa Zambia Mheshimiwa Kenneth Kaunda kuomboleza kifo cha mkewe, Mama Betty Kaunda (pichani), ambaye alifariki dunia Jumanne wiki hii akiwa na umri wa miaka 84.

“Nimesikitishwa na kushtushwa sana na taarifa za kifo cha Mama Betty Kaunda kilichotokea wiki hii mjini Harare, Zimbabwe, ambako alikuwa anamtembelea binti yake, Mama Musata Kaunda Banda.
Mama Betty Kaunda alikuwa shujaa wa Bara letu na mama wa mfano siyo kwa wananchi wa Zambia bali kwa Waafrika sote. Kifo chake ni pigo siyo kwako tu Mheshimiwa Rais, ama kwa wanafamilia, ama hata kwa wananchi wa Zambia bali kwa Waafrika wote”.

Rais Kikwete amesema katika salamu zake hizo, “Kwa miaka yote alipokuwa mke wa Rais wa Zambia tokea Oktoba 1964 hadi Novemba 1991, Mama Betty Kaunda alikuwa nguzo ya familia na nguzo yako Mheshimiwa Rais katika mapambano ya kuleta uhuru wa Zambia na katika harakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Mchango wake hautasahauliwa na pengo la kifo chake litabakia nasi kwa miaka mingi”.
“Mzee wangu Mheshimiwa Rais Kaunda nakutumia wewe salamu za dhati ya moyo wangu kufuatia kifo cha mama yetu na kupitia kwako kwa wanafamilia wote kwa kuondokewa na mhimili mkubwa wa familia.Naungana nanyi kuomboleza kifo cha mama yetu na pia naungana nanyi kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema peponi roho ya Marehemu Betty Kaunda. Amen”.

Mama Kaunda ambaye ameacha watoto wanane, wajukuu 30 na vitukuu 11, alizaliwa Novemba 1928 katika Jimbo la Kaskazini mwa Zambia wakati huo ikiitwa Northern Rhodesia, akaolewa na Mzee Kaunda mwaka 1946 na karibuni walisherehekea miaka 66 ya ndoa yao mjini Lusaka, Zambia.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Dar es Salaam.

21 Septemba, 2012

recommend to friends
  • Google+
  • PrintFriendly